MZUNGUKO WA HEDHI, SIKU ZA HEDHI (BLEED), SIKU SALAMA, SIKU ZA HATARI NA SIKU ZA UZAZI (MIMBA)
WHEEL OF FORTUNES
Katika mizunguko yangu ya kutoa ushauri wa afya kwenye mahusiano nimekutana na
watu wengi ambao ninagundua ya kwamba hawajui kuhesabu siku zao za hedhi au
hawajui mzunguko wao ni wa siku ngapi. Wanaume wengi ndio hawajui kabisa. Hivyo nimeamua kuandika japo kidogo kuhusu uhesabuji wa siku za hedhi.
BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE NA VIJANA WA LEO KUTOKUJUA KUHESABU
SIKU ZAO ZA HEDHI.
1- Kupotea kwa elimu ya jando katika makabila yetu
2- Kupotea kwa elimu ya afya katika mashule na nyumba za kuabudia
3- Kuwa na familia za kisasa zisizojali maisha ya kiasili ya kifamilia na
kujali zaidi maisha ya kisasa
4- Tabia mbaya kwa vijana kama vile ulevi, usagaji na ndoa za jinsia moja
5- Upatikanaji hovyo wa dawa za kuzuia mimba
6- Uvivu na uzembe wa kutokutaka kujifunza
7- Elimu isiyotolewa kwa mpangalio katika vyombo vya habari na katika mitandao
Kwa nini ni muhumi sasa uwe na uelewa mzuri wa wa Mzunguko wa Hedhi
1- Ili ujue siku zipi ni muhimu kwa ajili ya kupata mtoto
2- Ili ujue namna ya kuzuia kupata mimba zisizotarajiwa3- Kuwa Origino
JE UNAANZIA WAPI KUHESABU SIKU YA KWANZA YA MZUNGUKO WAKO?
Vifaa
- Kalenda
- Peni Nyekundu na Nyeusi#01 Mzunguko wa kawaida wa hedhi ni siku 28 – 32.
#02 Kama zitakuwa chini ya siku 28
hadi 21 basi huo ni mzunguko mfupi.
#03 Kama zitakuwa zaidi ya 32 -35 huo ni
mzunguko mrefu.
Ili kujua mzunguko wako ni mrefu au ni mfupi ni LAZIMA upate
wastani wa mizunguko yako ya hedhi ya miezi mitatu au zaidi.
#04 Mzunguko wa chini ya siku 20 upo lakini sio mzuri na hautakusaidia kupanga ratiba yako vizuri.
#05 Na pia mzunguko wa zaidi ya siku 35 sio mzuri.
#06 Alafu kuna wale wasioeleweka kila mwezi mzunguko unabadilika mara unakuwa mrefu, mwezi mwingine mfupi na mwingine wa kawaida.
DOKEZO MUHIMU: Mzunguko wa hedhi hata uwe mrefu, mfupi au wa kawaida au hata usiokuwa unaeleweka bado unayo nafasi ya kushika mimba, wapo wanawake wengi tu wenye mizunguko isiyoeleweka na wana watoto.
MAMBO MAKUU MAWAILI -2- YA KUZINGATIA UNAPOANZA KUHESABU NA KUJUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
1- Anza kuhesabu mzunguko wa hedhi yako kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi
yako (weka alama au zungushia tarehe hiyo na peni nyekundu - kwenye kalenda yako)
2- Na kisha malizia na siku moja kabla ya kupata hedhi nyingine ya mwezi
mwingine.
3- Mfano umepata hedhi leo tarehe 8/6/2017 basi nenda katika kalenda yako andika/zungushia tarehe nane kama siku
ya kwanza ya mzunguko wako wa hedhi, kisha subiria mpaka unapopata hedhi nyingine, kama utapata hedhi
nyingine tarehe 06 mwezi wa saba mana yake mzunguko wako wa hedhi wa mwezi wa sita umeisha
tarehe 05 mwezi wa 7 na ni mzunguko wa siku 28
MAKUNDI
MATATU YA SIKU ZA ZAKO NDANI YA MWEZI
Ili tuelewane vizuri tutatumia mzunguko wa wastani wa siku 28 ambao
umegawanyika katika makundi matatu
⇛ Siku
za hedhi, zinaitwa siku za damu
⇛ Siku za Mimba, zinaitwa siku za Hatari au siku za
Uzazi
⇛ Na Siku Zisizokuwa za Kupata Mimba, zinaitwa siku
salama
Siku yako ya kwanza ya mzunguko wako wa mwezi ndio siku ya kwanza ya umepata hedhi. Usihesabu kuanzia na siku umemaliza hedhi.
#01: Siku za hedhi au SIKU ZA DAMU katika
mzunguko wa siku 28 huwa ni 4-5. Hesabu kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi
mpaka siku ya mwisho ya kutokwa damu. Zinakuwa siku 4 hadi siku 5 lakini
zinaweza badilika hadi 7
#02: Baada ya kumaliza siku 4-5-7 za damu, siku
ya 6 hadi 10 NI SIKU AMBAZO kupata mimba NI VIGUMU, ingawa inaweza kutokea
ukapata ujauzito. Hizo huitwa siku salama. Pia siku ya 19 hadi siku ya 28 ni
siku ambazo sio rahisi au tuseme kwa ujumla haiwezekani kupata ujauzito. Hizo
pia huitwa siku salama
#03: Siku ya 10 hadi ya 18 ni siku zenye
UWEZEKANO MKUBWA wa kupata mimba. Katika siku hizi kama wewe unatafuta mtoto na
huna matatizo yeyote ya kiafya basi inafaa kuongeza bidii katika tendo la ndoa
ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito. Hizi huitwa siku za hatari au siku
za uzazi.
⇛ Siku
za hedhi, zinaitwa siku za damu
⇛ Siku za Mimba, zinaitwa siku za Hatari au siku za Uzazi
⇛ Na Siku Zisizokuwa za Kupata Mimba, zinaitwa siku salama
Siku yako ya kwanza ya mzunguko wako wa mwezi ndio siku ya kwanza ya umepata hedhi. Usihesabu kuanzia na siku umemaliza hedhi.
⇛ Siku za Mimba, zinaitwa siku za Hatari au siku za Uzazi
⇛ Na Siku Zisizokuwa za Kupata Mimba, zinaitwa siku salama
Siku yako ya kwanza ya mzunguko wako wa mwezi ndio siku ya kwanza ya umepata hedhi. Usihesabu kuanzia na siku umemaliza hedhi.
#01: Siku za hedhi au SIKU ZA DAMU katika
mzunguko wa siku 28 huwa ni 4-5. Hesabu kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi
mpaka siku ya mwisho ya kutokwa damu. Zinakuwa siku 4 hadi siku 5 lakini
zinaweza badilika hadi 7
#02: Baada ya kumaliza siku 4-5-7 za damu, siku
ya 6 hadi 10 NI SIKU AMBAZO kupata mimba NI VIGUMU, ingawa inaweza kutokea
ukapata ujauzito. Hizo huitwa siku salama. Pia siku ya 19 hadi siku ya 28 ni
siku ambazo sio rahisi au tuseme kwa ujumla haiwezekani kupata ujauzito. Hizo
pia huitwa siku salama
#03: Siku ya 10 hadi ya 18 ni siku zenye
UWEZEKANO MKUBWA wa kupata mimba. Katika siku hizi kama wewe unatafuta mtoto na
huna matatizo yeyote ya kiafya basi inafaa kuongeza bidii katika tendo la ndoa
ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito. Hizi huitwa siku za hatari au siku
za uzazi.
NINI
HUTOKEA KATIKA MZUNGUKO HUU?
Kawaida ukipata hedhi basi jua ya kwamba yai lako lilokuwa limekomaa limekosa
mbegu ya kiume hivyo ule ukuta uliokuwa umejengwa na damu kwa ajili ya kupokea
mtoto na kumkuza umebomoka…. Baada ya hapo mwili unaanza kuandaa yai lingine la
mwezi unaofuata.
NOTE 1 – Tangu yai kutoka katika mfuko wake linaweza kukaa masaa 12 hadi siku 1 (masaa 24) likiwa bado linauwezekano wa kurutubishwa na mbegu ya kiume na kuanza kuunda
mtoto.
NOTE 2 – Mbegu za kiume zinaweza kaa siku 3 hadi siku 4 zikiwa na uwezo wa kurutubisha yai la uzazi.
NOTE #1 na NOTE #2 ni muhimu kuzifahamu ili ujue ya kwamba unaweza kosea masaa
kadhaa na ukakosa kupata mimba hata kama huna matatizo yeyote ya kiafya au
matatizo ya mzunguko wa hedhi. Ndio mana unatakiwa uwe na bidii sana katika
tendo la ndoa kuanzia siku ya 11 hadi ya siku ya 18. Na hapa swala la urijali
wa mwanaume ni muhimu pia kwa kuwa kama mwanaume utakuwa na mbegu hafifu (infertile and low spermcont) zisizokuwa na mbio, mbegu chache, mbegu zenye kukaa muda mfupi na ambazo
hazijakomaa vizuri basi ni rahisi sana kuyakosa masaa hayo ya uhai wa yai.
KWA NINI SIKU ZA HEDHI HUBADILIKA BADILIKA.
Katika maisha ya sasa ni rahisi sana siku za hedhi kubadilika kwa sababu
mbalimbali lakini sababu kuu ni
(1) hali ya hewa (mabadiliko ya nchi au kusafiri)
(2) magonjwa na dawa kali za magonjwa
(3) kuvurugika kwa homoni
(3) msongo wa mawazo na
unene uliopitiliza.
(4) Sababu zingine ni pamoja na hizi:
- Historia ya kutumia madawa makali ya uzazi wa mpango
- Ulevi, uvutaji sigara na madawa ya kulevya
USHAURI KUTOKA HEALTH POINT
1- Kumbuka ya kwamba unaweza kukosa kushika mimba kwa muda hata wa miezi sita
lakini wewe na mwenzio mkawa wazima wa afya.
2- PUNGUZA UNENE: Kama wewe ni mnene na una matatizo ya hedhi, Ukifanikiwa
kupunguza uzito, utakuwa umemaliza asilimia kubwa ya matatizo ya hedhi.
3- Acha kabisa kutumia perfume, vipodozi na madawa ya kuongeza maumbile.
4- TUMIA PEDI ZA NEPLILY. Pedi hizi zimekuwa mkombozi kwa wanawake wengi wa
kipato cha chini. Pedi za nepilily ni dawa na ni pedi. Kwa sasa zipo Arusha,
DSM, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Lindi na Mbeya. Kama
utapenda kuwa wakala Karibu WASILIANA NAMI KWA SIMU 0752 693 692 au 0655 580
788
MZUNGUKOWA HEDHI - SIKU YA UZAZI
#KiundaniSiku za uzazi ni siku ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mimba, ni siku 4 kabla ya siku ya yai kutoka/kupevuka.
Kawaida yai hupevuka siku 14 kabla ya ya siku ya bleed.
Hii ni siku muhimu sana kwa wana ndoa kuijua.
Siku hii yai huwa linakuwa limeshakomaa na tayari limeshatoka katika nyumba
yake ya mayai (ovaries) na kuelekea katika mirija ya uzazi (fallopian tube) tayari kukutana na mbegu ya
kiume. Na kumbuka mbegu za kiume huishi muda wa masaa angalau 72 kwa hiyo muda wowote ndani ya masaa 72 kabla ya yai kutoka katika ovaries mtwanamke anaweza kudungwa mimba. Mfano kama yai linatoka tarehe 13, basi ukifanya tenbdo la ndoa siku ya tarehe 13,12,11,10 zote unaweza pata mimba - kwa hiyo hizi huitwa siku za mimba (fertile days), tofautisha na siku za hatari ambazo ni kuanzia siku yai limetoka na siku kadhaa baada ya yai kutoka.
KWA NINI BAADHI YA WANANDOA HUCHELEWA KUTUNGA MIMBA?
Kupata mtoto ni majaliwa ya mwenyezi Mungu lakini inaweza pia sababishwa na
baadhi ya mambo kama vile yalivyoorodheshwa hapa chini. Hizi ni baadhi ya
sababu, ili upate uhakika unatakiwa uende hospitalini na upime.
1- MAISHA MAFUPI YA YAI LA KIKE.
Yai likitoka katika nyumba ya mayai na
kuelekea mirija ya uzazi hadi kizazi linaweza ishi masaa kuanzia12 hadi 24+.
Mfano yai limotoka saa1 asubuhi na wewe ukakutana na mwenza wako saa5 usiku.
Ikiwa yai lako linauhai wa masaa12 hilo yai mbegu za kiume zitalikuta limesha
pooza. Lakini kama lina uhai wa masaa 20 basi kuna uwezekano mkubwa wa kutunga
mimba. Nini cha kufanya kama unahangaika kupata mimba hakikisha unazitumia vizuri siku za uzazi, ikiwezekana fanya tendo la ndoa usiku na asubuhi - amka na BBC. Baadhi ya dawa za tiba mbadala zimeonyesha kuwa na uwezo wa kutibu matatizo ya mayai kutokomaa vizuri
2- MBEGU ZA KIUME HAFIFU/DHAIFU/CHACHE.
Mbegu zinaweza kuwa hazina mikia na
hazina nguvu na haziwezi kuogelea hadi kuliwahi yai. Mshindo mmoja unaweza
kutoa mbegu karibia au zaidi ya milioni40. Mbegu hizo hushindana ili kuliwahi
yai, ni ile mbegu bora tu ndio itafika mapema.Kama mbegu ni chache (chini ya milioni 10 kwa mshindo mmoja) basi
uwezekano wa kuwa na mbegu bora nyingi unakuwa mdogo.
3- VIZUIZI KAMA UVIMBEE KWENYE MIRIJA YA UZAZIUvimbe unazuia yai na mbegu za
kiume kukutana kirahisi. Uvimbe unaweza jitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa na hali ya hewa au uvimbe tu usiojulikana kama endometriosis
4- UCHACHU MKALI KWENYE UKE (ASIDI NYINGI)uchachu mkubwa unaua mbegu nyingi
za kiume, hivyo kupunguza idadi ya mbegu zenye uwezo wa kuliwahi yai.
5- UCHAFUuchafu na ute mzito ndani ya kizazi huzifanya mbegu kushindwa
kuogelea na kuwahi kurutubisha yai
6- MALANGO WA UZAZI KUTOKUFUNGUKA (CERVIX) – Mlango kati ya uke na mji wa mimba
usipofunguka na kuruhusu mbegu kupita inachangia pia kuchelewa kupata ujauzito.
7- MVURUGIKO WA HOMONI.
Baadhi ya homoni kutofanya kazi vizuri. Homoni ndio
zinaamrisha mwili kufanya kazi zote za uzazi tangu kuamrisha yai litoke,
lipasuke na pia lijishikize kwenye mji wa uzazi. Pia homoni ndio zinachochea
viamshi vya tendo la ndoa. Kama homoni zimevurugwa basi mambo yako
yatavurugika.
DALILI ZA SIKU ZA UZAZI
1- UTE UTE UKENI - Ukikaribia siku zako za uzazi yaani yai ndio linajiandaa
kutoka katika mji wa mayai basi kunakuwa na mabadiliko ya ute ukeni, siku za
mwanzo kunakuwa na ute mzito, siku ya uzazi (yai limetoka) kunakuwa na ute
unaonasa kama utauvuta unavutika na siku zinazofuata baada ya yai kutoka ute
unakuwepo lakini unakuwa mgumu kama mtindi.2- JOTO KUONGEZEKA- Joto la mwili linaweza ongezeka kuanzia siku kabla yai
halijatoka na linakuwa juu zaidi siku yai limetoka. Kama unapima joto pima asubuhi
kabla hujaamka kitandani.
3- MLANGO WA UZAZI KUWA LAINI – Mlango wa uzazi upo kati ya nyumba ya uzazi na
uke. Mlango huu kawaida huwa mgumu kama pua, lakini siku yai likitoka unakuwa
mlaini kama shavu au lips na pia hupanuka kidogo na kusogea zaidi kwenye uke.
Wakati huu pia mlango huu huwa ni rahisi kufunguka.
4- HAMU YA TENDO LA NDOA KUONGEZEKA – Wanawake wengi katika siku hizi huwa
wachangamfu sana kwa tendo la ndoa. Mwanaume inatakiwa uwe mwelewa pindi
mwenzio anapokusogelea uchangamke mana ukizubaa unapoteza ramani ya uzazi.
5- MAZIWA KUWA LAINI.
6- UWEZO WA KUNUSA VITU VINGI HUONGEZEKA – Wanawake wengi huwa na uwezo mkubwa
wa kunusa na kuelewa harufu za vitu vingi sana wakati wakiwa period.
7- MAUMIVU UPANDE MMOJA WA KIUNO – wengine pia hupata maumivu upande mmoja wa
tumbo la uzazi. Kama dalili hii itaambatana na dalili zingine hapo juu na pia
inaangukia siku ambayo umeikadiria ndiyo ya uzazi basi una uhakika hiyo ni ndio
siku yenyewe.
8- Kuna dalili nyingine nyingi lakini si za jumla kwa watu wengi zinakuwa kwa
watu wachache wachache kama kuumwa kichwa na kujisikia vibaya
HEALTH POINT +255 752 693 692
Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi.
(1) Kujua mzunguko wako wa hedhi vizuri
(2) Kujua siku za uzazi (tuma meseji yako yenye tarehe za kuanza bleed kila mwezi - ukijitambulisha na kilo zako na umri wako na mahli unapoishi. AshaRose - Misungwi - Mwanza, miaka 28 kilo 80 - mfano 27/01/2017, 26/02/2017, 25/03/2017 na 29/04/2017
(3) kama umeshapima na kukutwa na matatizo ya ovaries na ukosefu wa homoni basi unaweza wasiliana nasi pia kwa kupata tiba mbadala
(4) Kubalansi homoni
(5) Kupunguza Unene na Uzito Uliozidi
(6) Ushauri wa chakula kwa watu wenye kisukari aina ya II
(7) Matumizi ya pedi
za kisasa za Neplily zinazoondoa miwasho, uchafu na fangasi ukeni pia kutibu
UTI
ONYO:
SISI TUNAFUNDISHA WATU WAJITAMBUE (KUJUA DALILI) NA KISHA UENDE HOSPITALI
KUPIMA ALAFU NDIO UPEWE TIBA.
Jamani mi siku zangu hazieleweki kila mwezi unasiku tofauti mpka napata wasiwasi wakati wa tendo la ndoa na mfano mwezi uliopita nimeingia tarehe 14/2 je nikifanya tendo la ndoa kuanzia tarehe 10/3naweza pata ujauzito
ReplyDeleteJamani mi siku zangu hazieleweki kila mwezi unasiku tofauti mpka napata wasiwasi wakati wa tendo la ndoa na mfano mwezi uliopita nimeingia tarehe 14/2 je nikifanya tendo la ndoa kuanzia tarehe 10/3naweza pata ujauzito
ReplyDelete